Msemakweli
GAZETI LA KIKRISTO LA KILA WIKI
HABARI/TANGAZO
CFDs taifa yazindua kalenda na tovuti
Na Uunique
Maringo
Jumuia ya Watetezi wa Imani, The Community of faith
Defenders (CFDs) wa Kanisa la Pentecostal Holiness Mission (PHM) imezindua
kalenda mpya ya mwaka 2017, tovuti ya Kanisa na blog kwa ajili ya kurahisisha
utendaji wa kazi ndani ya makanisa yote ya PHM.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Manzese Jijini Dar
es Salaama lililopo Kanisa hilo na Mgeni Rasmi ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Iringa Dakta Given Msomba kwa kushirikiana na Ofisi ya Akofu Mkuu PHM,
Baraza la Waangalizi la PHM, Wajumbe wa Bodi ya PHM, Askofu wa Jimbo la
Mashariki, wachungaji, wenyeviti wa CFDs Majimbo yote, Dkta Msomba alisema kuwa
kutokana na teknologia kukua kwa kasi ni jukumu la kila Kanisa kuachana na
mfumo wa analogia na badala yake kuingia katika mfumo wa teknolojia ya digitali
ili kurahisisha kazi za kanisa kwenda katika hali inayohitajika.
Alisema kitendo cha Kanisa hilo kuamua kuzindua kalenda
mpya ya mwaka 2017 sambamba na kuanzisha tovuti kitasaidia makanisa yote ya PHM
ulimwenguni kupata taarifa kwa wakati muafaka badala ya mfumo ule wa awali wa
barua ambayo ulikua unachelewa kufikia walengwa kwa wakati.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa,
Dk. Given Msomba (kulia) akizindua kalenda ya Kanisa la PHM. Anayefuatia kutoka
upande wake wa kulia ni Katibu Mkuu wa CFDs Taifa Bw. Daima Kabogo, Askofu wa
PHM Jimbo la Mashariki, Eliya Kiputa na Mwenyekiti wa Taifa, Mchungaji
Emmanueli Mwangwale.
Aidha katika risala yao kwa Mgeni Rasmi, Katibu wa
CFDs Taifa Bwana Daima Kabogo alisema kuwa tovuti hiyo ya Kanisa inajulikana
kama www.phmtz.org na blog ya Idara iitwayo cfdstz.blogspot.com
Katibu huyo alifafanua kuwa CFDs ni Watetezi Imani
kama maandiko yanavyosema katika 1Yohana 2:14b kuwa “Nimewaandikia ninyi vijana kwa
sabababu mna nguvu na Neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule
mwovu.”
Aliongeza kuwa CFDs wameamua kwa dhati kutangaza
Neno la Mungu ulimwenguni kote kwa njia mbalimbali, kianalogia na kidigitali
kwa kutumia teknolojia katika kutii agizo la Bwana Yesu Kristo katika Marko
16:15. “Enendeni ulimwenguni mwote mkahubiri Injili kwa kila kiumbe.”
Katibu Kabogo alisema kuwa Idara ya CFDs ina malengo
ya jumla ambayo anatamani yafanikiwe ili ufalme wa Mungu upate kujengwa kisha
Mungu kujipatia utukufu kupitia kujifunza Biblia, kufanya maombi na maombezi
kwa watu wenye shida mbalimbali, kuwasaidia vijana kuishi maisha matakatifu,
kushuhudia kueneza Injili na kutoa huduma za kijamii.
Alisema mwelekeo wa Idara ya CFDs ni kuwajibika
ipasavyo kwa wana Idara wake kupitia uongozi uliopo ili kuleta maendeleo yenye
tija ndani ya Idara yanayolenga ukuaji wa Kanisa la PHM kiroho na kiuchumi kwa
kutumia rasilimali zilizopo. Katibu huyo alisema.
Baada ya uzinduzi wa kalenda ya mwaka 2017
iliyotengenezwa na PHM mzaliwa wa kwanza alinunuliwa kwa shilingi laki tatu
ambapo wageni waalikwa, wachungaji na watumishi walinunua kalenda hiyo kwa
shilingi laki moja
Kalenda hiyo inaendelea kupatikana katika makanisa yote
ya PMH.
No comments:
Write comments