Jumuiya ya Watetezi wa Imani - Community of Faith
Defenders (CFDs) ni moja ya Idara ndani ya kanisa la Pentecostal Holiness Mission (PHM)
yenye malengo chanya kwa
kanisa kama Idara zingine. Hii ni idara ambayo inayohusisha
vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 50. Idara ya CFDs katika utendaji
wa kazi imegawanyika katika ngazi nne, kuanzia ngazi ya chini yaani kanisa la
mahali hadi ngazi ya juu ya kitaifa kama ifuatavyo:- CFDs
katika kanisa la mahali, Sehemu (Section), Jimbo na Taifa.
Idara
ya CFDs kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia mwaka 2017 hadi 2027 imekuwa na
malengo makuu kadha ya kimkakati. Katika utekelezaji wake wa majukumu hayo ya
kimkakati, CFDs unahusisha uongozi wa Taifa, Majimbo, Sehemu, Makanisa ya
mahali na wana CFDs wote kwa ujumula nchini. Ili kulifanikisha zoezi zima hili tumesimamia
kauli mbiu yetu inayosema “Mabadiliko ya kiroho na kiuchumi katika PHM
na CFDs inawezekana!! Wajibika!!” Lengo likiwa ni kuwajibika
ipasavyo kwa kila mwana Idara kupitia uongozi uliopo ili kuleta maendeleo yenye
tija ndani ya Idara. Hii ni kulingana na vipaumbele maalumu vya utekelezaji vya
kimkakati vilivyowekwa kwa miaka hiyo. Hali hii inalenga ukuaji wa kanisa
kiroho na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi zaidi.
Monday, October 24, 2016
Jumuiya ya Watetezi wa Imani - Community of Faith Defenders (CFDs)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Pentecostal Holiness Mission (P.H.M), is a non-Profit Christian denomination, an organization which is based on preaching the True Go...
-
(MGCC) Mount of God Conference Center ni mradi wa ukumbi mkubwa wa PHM - Pentecost Holiness Mission, unaojengwa Mkoa wa Iringa chini...
-
MATUKIO YA CFDs KITAIFA KWA MWAKA 2017 1. 16-20 Januari 2017 Maombi Ya Kitaifa 2. 28 January 2017 ...
-
Mount of God Conference Center (MGCC) - UKUMBI Mount of God Conference Center ni mradi wa ukumbi mkubwa wa PHM - Pentecost Holiness Miss...
-
CFDs Jumuiya ya Watetezi wa Imani - Community of Faith Defenders (CFDs) ni moja ya Idara ndani ya kanisa la Pentecostal Holiness Mi...
-
ZIALA NA KAZI KATIKA ENEO LA KUJENGA UKUMBI WA KISASA WA MGCC
2 comments:
Write commentsVery good. Thank you. You have done a good job. May God bless you
ReplyDeleteVery good. Thank you. You have done a good job. May God bless you
ReplyDelete