MGCC Front View
KARIBU SANA KATIGA BLOG HII- YOU ARE ALL WELCOME
CFDs National Leadership
MGCC Side to Front View
MGCC Side view

Wednesday, December 28, 2016

Gazeti la Jibu Jumapili, Novemba 6-12, 2016, Ukurasa wa 6



Jibu
                                                         la Maisha
Mhadhiri chuo kikuu atoa mbinu kuwanusuru vijana
·       Ataka kanisa kuingilia kati
·       Awapa kazi viongozi wa dini, wachungaji
Na Samweli Thomas

Kufuatia kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili, hususani kwa vijana wa Tanzania na kusababisha kwa kuibuka kwa makundi tishio, Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Iringa, Dk. Given Msomba, ametoa mbinu za kuwanusuru na majanga hayo.
Dk. Msomba alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Kalenda na Tovuti ya Kanisa la Pentecostal Holiness Mission, uliofanyika katika Kanisa hilo wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri huyo aliweka wazi kuwa, zipo mbinu kadha wa kadha za kuwanusuru vijana wa Tanzania, wanao tangatanga mitaani, huku baadhi wakijiingiza katika makundi ya kihalifu.
Akitaja baadhi ya mbinu hizo alisema, ni kuwahubiria Habari Njema za Yesu Kristo, na kuwafundisha kuachana na mambo maovu.
Mbinu nyingine alisema, ni kuwapa vijana elimu ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na kuwafungulia miradi ambayo wanaweza kuendesha wao wenyewe na kwamba kwa kufanya hivyo wimbi la vijana wa mitaani litapungua.
Pamoja na hilo aliwataka wazazi kuwajibika katika malezi kwa watoto wao, huku akiongeza kuwa chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili kwa watoto walio wengi ni wazazi.
Alisema kuwa wazazi wameshindwa kutimiza wajibu wao na kwamba hali hiyo imepelekea vijana wengi kuharibika na baadhi yao kukimbia nyumbani na kujiingiza katika makundi ya kihalifu.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa, Dk. Given Msomba (kulia) akizindua kalenda ya Kanisa la PHM. Anayefuatia kutoka upande wake wa kulia ni Katibu Mkuu wa CFDs Taifa Bw. Daima Kabogo, Askofu wa PHM Jimbo la Mashariki, Eliya Kiputa na Mwenyekiti wa Taifa, Mchungaji Emmanueli Mwangwale.
Kutokana na hilo akawataka wazazi kutobweteka na kwamba wawafatilie watoto wao katika kila wanachokifanya, ili kuwanusuru vijana kujiingiza katika makundi hatarishi hata kupelekea wengine kupoteza maisha kutokana na unyang’anyi.
Sambamba na hilo aliwataka viongozi wa dini nchini, kutambua kuwa wao ndio wameibeba Tanzania na kwamba amani ikitoweka, watakuwa chanzo, hivyo akawakumbusha kuzidi kumlilia Mungu anusuru Taifa la Tanzania na matukio ya kiharifu yanayojitokeza.
Dk. Msomba akawataka vijana wa Tanzania kutokubali kubweteka, bali watumie fursa zilizopo nchini katika kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na utegemezi.
Alisema kuwa ikiwa vijana watajikita katika kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha miradi mbalimbali ni dhahiri kuwa hakutakuwa na makundi ya kihalifu kama vile panya road na mengineyo.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo wa Kalenda ya Idara ya mwaka 2017, Tovuti ya Kanisa na Blogspot, Katibu wa Idara ya Jumuia ya Watetezi wa Imani CFDs, Bw. Daima Kabogo, alisema hatua hiyo waliyofikia ni Mungu amekuwa pamoja nao.
Alisema kuwa, Idara hiyo inazidua tovuti ya Kanisa la PHM ya www.phmtz.org, blog ya Idara iitwayo cfdstz.blogspot.com, pamoja na Kalenda ya mwaka 2017 na kwamba lengo likiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili kuifanya kazi ya Mungu.
Akitaja baadhi ya malengo ya Idara hiyo alisema ni pamoja na; Kujifunza Biblia, kufanya maombi na maombezi kwa wenye shida mbalimbali, kuwasaidia vijana kuishi maisha matakatifu, kushuhudia, kueneza Injili (kuhubiri), kutoa na kujitoa, kuwa waaminifu kwa Mungu, Kanisa na jamii, kutunza wakati na huduma za kijamii kama vile kujenga shule, vituo vya afya na kumbi za mikutano.
Malengo mengine alisema ni Ujenzi wa Mount of God Conference Center (MGCC) na Ujenzi wa Mount of God Seminary (MGS), ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya muda mrefu na muda mfupi na kwamba Mungu atafanikisha malengo yao.
Bw. Kabogo aliwataka waumini wa Kanisa hilo na watanzania kwa ujumla, kununua Kalenda za Kanisa hilo, kutembelea Tovuti, pamoja na blog ya Idara hiyo kwa lengo la kijifunza mambo kadha wa kadha yatakayo waimarisha kiroho.
Kwa upande wa Askofu wa PHM Jimbo la Mashariki, Eliya Kiputa, akizungumza wakati wa hafla hiyo aliwashukuru viongozi wa Idara hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya na kwamba Mungu atazidi kuwainua.
Aliwataka vingozi wa Idara hiyo kudumisha umoja na mshikamano ili waweze kufika mbali na kutimiza malengo waliyojiwekea kama Idara.
Kisha akalitaka Kanisa kuwatia moyo kwa kununua Kalenda za Kanisa hilo, ikiwa ni pamoja na kutembelea tovuti pamoja na blog ya Idara hiyo.
Viongozi wa Idara hiyo ni Emmanueli Mwangwale, ambaye ni mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti ni Deo Mgimbe, Katibu ni Daima Kabogo, Katibu Msaidizi ni Tito Mwasyove na Mweka Hazini ni Ferdnand Mlandali na Mweka Hazina Msaidizi ni Jamesi Mwampamba.


Popular Posts