Jibu
la Maisha
Mhadhiri chuo kikuu atoa mbinu
kuwanusuru vijana
· Ataka kanisa kuingilia kati
· Awapa kazi viongozi wa dini, wachungaji
Na
Samweli Thomas
Kufuatia
kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili, hususani kwa vijana wa Tanzania na
kusababisha kwa kuibuka kwa makundi tishio, Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Iringa,
Dk. Given Msomba, ametoa mbinu za kuwanusuru na majanga hayo.
Dk.
Msomba alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Kalenda na Tovuti ya Kanisa la
Pentecostal Holiness Mission, uliofanyika katika Kanisa hilo wiki iliyopita Jijini
Dar es Salaam.
Mhadhiri
huyo aliweka wazi kuwa, zipo mbinu kadha wa kadha za kuwanusuru vijana wa
Tanzania, wanao tangatanga mitaani, huku baadhi wakijiingiza katika makundi ya
kihalifu.
Akitaja
baadhi ya mbinu hizo alisema, ni kuwahubiria Habari Njema za Yesu Kristo, na
kuwafundisha kuachana na mambo maovu.
Mbinu
nyingine alisema, ni kuwapa vijana elimu ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na
kuwafungulia miradi ambayo wanaweza kuendesha wao wenyewe na kwamba kwa kufanya
hivyo wimbi la vijana wa mitaani litapungua.
Pamoja
na hilo aliwataka wazazi kuwajibika katika malezi kwa watoto wao, huku
akiongeza kuwa chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili kwa watoto walio wengi
ni wazazi.
Alisema
kuwa wazazi wameshindwa kutimiza wajibu wao na kwamba hali hiyo imepelekea
vijana wengi kuharibika na baadhi yao kukimbia nyumbani na kujiingiza katika
makundi ya kihalifu.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa,
Dk. Given Msomba (kulia) akizindua kalenda ya Kanisa la PHM. Anayefuatia kutoka
upande wake wa kulia ni Katibu Mkuu wa CFDs Taifa Bw. Daima Kabogo, Askofu wa
PHM Jimbo la Mashariki, Eliya Kiputa na Mwenyekiti wa Taifa, Mchungaji
Emmanueli Mwangwale.
Kutokana
na hilo akawataka wazazi kutobweteka na kwamba wawafatilie watoto wao katika
kila wanachokifanya, ili kuwanusuru vijana kujiingiza katika makundi hatarishi
hata kupelekea wengine kupoteza maisha kutokana na unyang’anyi.
Sambamba
na hilo aliwataka viongozi wa dini nchini, kutambua kuwa wao ndio wameibeba
Tanzania na kwamba amani ikitoweka, watakuwa chanzo, hivyo akawakumbusha kuzidi
kumlilia Mungu anusuru Taifa la Tanzania na matukio ya kiharifu yanayojitokeza.
Dk.
Msomba akawataka vijana wa Tanzania kutokubali kubweteka, bali watumie fursa
zilizopo nchini katika kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na utegemezi.
Alisema
kuwa ikiwa vijana watajikita katika kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha miradi
mbalimbali ni dhahiri kuwa hakutakuwa na makundi ya kihalifu kama vile panya
road na mengineyo.
Awali
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo wa Kalenda ya Idara
ya mwaka 2017, Tovuti ya Kanisa na Blogspot, Katibu wa Idara ya Jumuia ya
Watetezi wa Imani CFDs, Bw. Daima Kabogo, alisema hatua hiyo waliyofikia ni
Mungu amekuwa pamoja nao.
Alisema
kuwa, Idara hiyo inazidua tovuti ya Kanisa la PHM ya www.phmtz.org, blog ya Idara iitwayo cfdstz.blogspot.com, pamoja
na Kalenda ya mwaka 2017 na kwamba lengo likiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili kuifanya
kazi ya Mungu.
Akitaja
baadhi ya malengo ya Idara hiyo alisema ni pamoja na; Kujifunza Biblia, kufanya
maombi na maombezi kwa wenye shida mbalimbali, kuwasaidia vijana kuishi maisha
matakatifu, kushuhudia, kueneza Injili (kuhubiri), kutoa na kujitoa, kuwa
waaminifu kwa Mungu, Kanisa na jamii, kutunza wakati na huduma za kijamii kama
vile kujenga shule, vituo vya afya na kumbi za mikutano.
Malengo
mengine alisema ni Ujenzi wa Mount of God Conference Center (MGCC) na Ujenzi wa
Mount of God Seminary (MGS), ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ya muda mrefu
na muda mfupi na kwamba Mungu atafanikisha malengo yao.
Bw.
Kabogo aliwataka waumini wa Kanisa hilo na watanzania kwa ujumla, kununua
Kalenda za Kanisa hilo, kutembelea Tovuti, pamoja na blog ya Idara hiyo kwa
lengo la kijifunza mambo kadha wa kadha yatakayo waimarisha kiroho.
Kwa
upande wa Askofu wa PHM Jimbo la Mashariki, Eliya Kiputa, akizungumza wakati wa
hafla hiyo aliwashukuru viongozi wa Idara hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya na
kwamba Mungu atazidi kuwainua.
Aliwataka
vingozi wa Idara hiyo kudumisha umoja na mshikamano ili waweze kufika mbali na
kutimiza malengo waliyojiwekea kama Idara.
Kisha
akalitaka Kanisa kuwatia moyo kwa kununua Kalenda za Kanisa hilo, ikiwa ni pamoja
na kutembelea tovuti pamoja na blog ya Idara hiyo.
Viongozi
wa Idara hiyo ni Emmanueli Mwangwale, ambaye ni mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti
ni Deo Mgimbe, Katibu ni Daima Kabogo, Katibu Msaidizi ni Tito Mwasyove na Mweka
Hazini ni Ferdnand Mlandali na Mweka Hazina Msaidizi ni Jamesi Mwampamba.